Tuesday, December 15, 2009

NAI PICS SEHEMU YA PILI..













Picha ya kwanza ndio highlight ya safari yangu Nai! Tulicheka kweli! Ailinda Sawe, Tanzanias Namba One designer, Mama Afrika Sana anashangaa Kishweng!
Katika picha nyingine, tunaangalia mfano wa boarding passes za njano! Tulizibeba hadi lango la kuchekiwa! Mmmmmh...

Nikisafiri huwa nahamu sana ya kukutana na wenyeji. Muda unakuwa mdogo. Hata hivyo namshukuru Ayan na wafanyakazi wenzake pale Moi International kwa kunipokea vizuri, kupiga nao picha sehemu ambayo ni nyeti. Zaidi kwa ukarimu wao!
Hope mtaniunganisha na momodo wa Nai!

Nilinunua majarida mbalimbali, nikagundua kwamba Nai kuna vyuo kibao vinavyofundisha maswala ya urembo!Nahisi Kenya itafika mbali sana katika miaka ya mbele kwenye maswala ya Mitindo maana Ms Kenya wala sio shindano lenye nguvu tena. Nahisi na hapa Tz, hali kama hiyo imeanza?

Kuna kitu kinaitwa "gene pool", kwa tafsiri zahisi, Tanzania inaelekea kuwa na gene pool yenye vigezo vya Kimataifa kwa wanamitindo katika mikoa ya Kilimanjaro na Mara.
Wasichana wa maeneo hayo huwa ni warefu na wenye uzuri wa kipekee. Fikiria Miriam Odemba!
Mikoa mingine wasichana wanakuwa wapana, wafupi wa wastani na rangi huwa ni changanyiko, weusi, maji ya kunde, brown na weupe wa kuungua.

Nairobi nilikuwa nawaona wasichana wenye tofauti kibao! Wengi wazuri kwa modeling ya kimagharibi!! Makabila machache yana wasichana wenye uzuri wa kipekee hadi wanashangaza! Si ajabu Imani alipatikana akikatiza mitaa ya Nai na leo ni historia katika ulimwengu wa mamodo weusi!

Hata hivyo, wanaume wengi wa nchi mbalimbali wakifika Dar huwa wanapigwa butwaa na uwingi wa aina za warembo wa nchi hii, nadhani ni kitu kizuri! Kwahiyo masisita wa Bongo, nawapa hongera, maana katika ufupi wenu, upana wenu, rangi mbalimbali na mchnagnyiko wa "genes", MNACHENGUA!

WATAMBUE MAMODO WA SHINDANO LA UNIQ KWA KARIBU











Monday, December 14, 2009

Ally Rehmtullah's Collection '2025' launch in Tunisia!!









MAMODO WA UNIQ....



Kionjo tu cha weekend bomba na mamodo wa Uniq, walipotembelea maduka ya wadhamini Truworths, kisha kupanda basi hadi Giraffe, kupata lunch na kupiga picha na waandishi....

MALE MODO



DEOGRATIUS NI MALE MODO MWENYEJI WA DAR NA SASA YUPO ARUSHA. MZOEFU WA MODELING. ANA BLOG YAKE(http://d-niceblogspot.blogspot.com)
YUPO TAYARI KWA MICHONGO MBALIMBALI!! Wasiliana nami nikupe contact zake.

JAMILLA VERA SWAI






JAMILLA VERA SWAI to represent SWAHILI FASHION WEEK.
MOZAMBIQUE AND SWAHILI FASHION WEEK COLLABORATION

Jamilla Vera Swai has been invited by Mozambique Fashion
Week, to represent Swahili Fashion Week at this Annual
Event to be Held in Maputo from 6-12 December 2009.
“It's a pleasure representing Tanzania and Swahili
Fashion Week at the Mozambique Fashion Week. I had wanted to
participate in International Events and my dreams shall now
Come true” says Jamilla
She was selected by International producer Jan Malan and
Mwamvita Makamba , Director of corpoarate Affairs Vodacom
Tanzania during the Swahili Fashion Week.
Speaking of her collection to be unveiled on 12 December
during the Pan African Showcase, “My collection is
inspired by nature. I've used shades of brown, beige, cream,
green, black and purple to emphasize this. Some darker dyes
bleed into lighter colors to mimic a soaked garment when you
walk on wet ground. The style is modern with an ethnic feel
to it” Swai adds
During Swahili Fashion 2009 in association with Vodacom
& ZTE designers Adelia and Sheila Tique from Mozambique
had the opportunity to participate in November this year.
This is just the Beginning of Strenghtening of Not only
Political ties between Tanzania and Mozambique but also
Cultural ties too. The Bond shall grow Deeper and stronger
Year after year.

ABOUT SWAHILI FASHION WEEK (SFW)

Swahili Fashion Week was founded by Mustafa Hassanali one
of Tanzania’s top Fashion designers and launched
successfully in November 2008.
Swahili Fashion week is a platform for designers, both
fashion and accessory from Swahili speaking countries to
showcase their creativity, market their art and networking
with their clientele all aimed at Promoting Fashion as an
income generating, Job creating industry while emphasizing
the " Made in Tanzania " concept.
Swahili Fashion Week is set to be an annual fashion
extravaganza where by both new and veteran designers can
showcase their work. It is also a venue for fashion lovers
to enjoy a few days of fabulous fashion creativity from
Tanzania and its neighbouring countries. Initiating a
dynamic and promising platform for the fashion industry in
Tanzania, The Swahili Fashion Week is geared towards being
the most sought out after Fashion platform in Eastern Africa
for the International market.

ABOUT JAMILLA VERA SWAI
Unless you are familiar with the local fashion industry you
most probably have not heard of Jamilla Vera Swai. This
young woman compensates her petite stature by making grand,
vibrant, exotic, all in your face extraordinaire designs. In
her designs, she caters for everyone, from the small ones to
the grown ups. There is nothing that this mother of one can
not do, and when you actually meet her you get to be
surprised by everything she has accomplished.
Born in a month of August in Dar es Salaam (a lady never
tells her age) to a predominant Dr. Swai and his lovely
wife Juliette (I can see where Jamilla gets her beauty from)
Jamilla’s love affair with fashion started when she was
just 7 years old. She would use her dolls to create clothes
for. At the age of 14, while she was still in high school,
as it usually happens she caught a modeling agency’s eye
and started modeling for adverts on local TV station in
Maputo as well as designing for the agency she was signed
with, The Studio Stilo.
Being of a petite stature and not being able to do modeling
full time, Jamilla concentrated on what she was doing best,
which was designing. To perfect her skills she joined
Institute de Bela Artes in Maputo to study fashion then
later on moved to Fashion College International in Nairobi
to complete her studies.
she decided to return to her home town of Dar es salaam,
open up Jamilla Vera Swai Design Studio and give the already
established local designers some very heavy competition.
Since then she has participated in various fashion shows and
did some exclusive designs for her growing group of clients,
including clothes for retail shops

ABOUT MOZAMBIQUE FASHION WEEK
The Mozambique Fashion Week (MFW), is an artistic and
cultural event, and is the only one in Mozambique that is
connected to the desire to create and that works in
discovering new talents and fashion designers, creating
opportunities in opening new business markets and
professional contacts for the fashion industry in Mozambique
andworldwide.
Mozambique Fashion Week has as an objective of enhancing
national fashion and beauty and also aims at expanding the
fashion market in Mozambique, discovering new talents around
the country.
The MFW is a driving vehicle for the development of the
Mozambican fashion industry and a major tourist attraction in the promotion of culture and well-being, putting
Mozambique in the itinerary of international fashion.
Mustafa Hassanali was the first designer to Represent
Tanzania at the Mozambique Fashion Week in 2007.

Wednesday, December 9, 2009

UWANJA WA NDEGE WA NAIROBI TORORO!






Sasa hivi nipo ndani ya chumba cha kusubiria ndege hapa Moi Int Airport. Tulitarajia kundoka hapa saa 4 kamili usiku. Tulifika uwanjani saa 2 kamili baada ya kuhangaika na foleni kali kutoka mjini!
Kwenye saa 3 hivi, lilipigwa tangazo likiwataka abiria wa ndege yetu kufika dawati la 'transfer' ambalo kwa kawaida huwa lina vurugu nyingi na wingi wa watu! Tulipanga foleni iliyojaa wahindi na wachina. Katika kudadisi, tuligundua wanaelekea Msumbiji lakini ndege yao ya kuunganisha ilikuwa imefutwa hadi Ijumaa! Duh!
Basi, msitari hauendi, watu kibao, nikamwomba mama mmoja tuliyekuwa naye amwombe mdada mhudumu atusaidie, kumbe ndio ikawa nafuu yetu kwani ndani ya dak 5, tukawa tumepata boarding passes mpya! Tukakimbilia haraka geti namba 4 ambapo ndipo nilipo naaandika haya kupitia simu yangu.

Wenzangu wametawanyika wanazurura, watu wamekaaa chini ama kulala, kumbuka lounge hizi hazina hata Tv jamani...tutaanza kuzoeana hapa, si unajua wabongo wakianza kuteta.....wahudumu staha zimewatoka sasa wanapiga stori hapa kama vile tupo Rose Garden!

Sababu? Tangazo linasema kwamba kuna 'anomaly', tetesi ni kwamba taa kwenye runway ya ndege haziwaki! Ni kweli, hakuna ndege zinazotua wala kuruka, ni kimya! Eneo la maegesho ya ndege ni giza tupu!

Nasikia njaa. Dereva keshanifuata Dar, nimepiga stori na mwenzangu hadi mistari imekwisha. Aaaah, tangazo lingine, sauti ya mwanadada anasema kuna tatizo kwenye runway, wanaomba radhi!

Mhhh, hawa wadada waliokuwa wanatukagua ni warembo, sijui watakubali kutoka kwenye Umodo........?

Habari ndio hiyo, ngoja nikawashangaze na Kiswahili propa!